Mkoa wa Dar unaongoza kwa biashara haramu ya Binadamu nchini - Waziri Lugola


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza nchini kwa kufanya biashara haramu ya kusafirisha binadamu huku akitoa onyo kali kwa wanaojihusisha na biashara hiyo.


Akizungumza kabla ya kufungua Mafunzo ya siku tano ya Watekelezaji wa sheria ya kuzuia biashara hiyo haramu, katika hoteli ya Ngalawa, mjini Unguja, Zanzibar, Lugola amesema wanaofanya kazi hiyo waiache mara moja maana Serikali itawashughulikia.

"Tatizo hili, linaweza onekana likawa dogo, lakini ukweli ni kwamba sote tunafahamu ni kubwa na limeendelea kukua kila mwaka. Uzoefu wa kiutendaji kutoka Sekretareti hususani kutokana na wahanga wanaookolewa unaonyesha kwamba biashara hii inafanyika sana Mkoa wa Dar es Salaam Tanga, Mwanza, Kigoma, Geita, Dodoma, Singida, Arusha, Manyara, Shinyanga na Tanzania Zanzibar,” alisema Lugola.

Lugola alisema licha ya changamoto hizo, lakini Serikali katika kipindi cha kuanzia Januari mpaka Disemba 2018 imefanikiwa kuwaokoa jumla ya Watanzania 147 waliokuwa wahanga wa biashara haramu ya usafirishaji binadamu. Kati ya wahanga 141walikuwa wakitumikishwa katika mikoa mbalimbali nchini.

Pia Lugola alisema wahanga 6 walikuwa wakitumikishwa nje ya nchi ambapo watano walikuokolewa kutoka Thailand na mhanga mmoja kutoka Malasia.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items