Kocha wa Simba aeleza walikuwa tayari kukutana na timu yoyote


Kocha wa timu ya Simba SC, Patrck Aussems ameeleza kuwa walikuwa tayari kukutana na timu yoyote wala walikuwa hawahofii droo ya robo fainali jana na wameshagundua cha kufanya kwenye mechi za ugenini.

Kocha huyo alisema kuwa Simba kwa sasa ni timu kubwa haipaswi kuhofia timu yoyote Afrika hususani kwenye robo fainali.

“Mpira una matokeo ya ajabu hasa kutokana na namna inavyokuwa baada ya dakikia tisini, nina imani na kikosi changu tutapata matokeo kwa timu yoyote.

“Ushindani ni mkubwa kwa kuwa hatua hii ni ngumu na kila timu ni bora, hesabu zetu ni kuona tunashinda katika michezo yetu na kufanyia kazi makosa ambayo tuliyafanya kwenye michezo yetu ya nyuma,” alisema Aussems.