3/15/2019

Mbowe atema nyongo 'Chama cha siasa ni kama dodoki linanyonya kila kitu'


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelea (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa Chama cha siasa ni kama dodoki linanyonya kila kitu.

Mbowe ameyasema hayo katika Mkutano wake na Vyombo vya habari huku akisema kuwa  Kiongozi kufanya siasa za upinzani ni mzigo mzito ambao unahitaji mtu mwenye moyo thabiti.

Akizungumzia kuingia kwa Lowassa ndani CHADEMA, Mbowe amesema chama cha siasa ni kama dodoki. Linanyonya kila kitu.

"Dodoki litanyonya maji safi kama litawekwa kwenye maji safi. Hivyo hivyo litanyonya maji taka kama litawekwa kwenye maji taka. CHADEMA ni chama cha siasa, tunahitaji wanachama," amesema Mbowe.