Loading...

3/19/2019

Mfahamu N! XAU-TOMA (Bush Man)

Kama uliwahi kufuatilia filamu ya ”THE GODS MUST BE CRAZY” Utagundua kwamba kuna mzee aliyekuwa anajulikana kama BUSH MAN ambae ndiye aliyekuwa mhusika mkuu katika filamu hiyo, Leo nimekuletea wasifu wake na maisha yake kwa ujumla.

Wasifu Wake.
N! XAU TOMA, Alizaliwa Desemba 16, 1944, alikuwa Mnamibia  na muigizaji ambaye alikuwa  akiishi porini, alikuwa maarufu baada ya uhusika wake kama Mhusika Mkuu  katika filamu ya THE GODS MUST BE CRAZY, Iliyoigizwa mnamo mwaka 1980 ambapo yeye alicheza kama mtu kutoka Jangwa la Kalahari, na watu wa Namibia walimfahamu yeye kama Muigizaji Maarufu kuliko wote Nchini Namibia.

N!xau alikuwa mwanachama wa SAN (Wenyeji wa Maeneo ya Jangwa la Kalahari), ambao pia walijulikana kama BUSH MEN. Alikua na uwezo wa kuongea kwa ufasaha Lugha au Makabila takribani matatu yanayopatikana maeneo ya Namibia yaani ki-Ju|’hoan, Ki- Otjiherero na Ki-Tswana

Kutokana na Mwenendo wa Maisha ya porini aliyoishi, yeye mwenyewe hakujua umri wake halisi, na kabla ya kuonekana  katika filamu ya THE GODS MUST BE CRAZY, Bush man alikuwa na uzoefu kidogo sana wa maisha ya kisasa, alikuwa amewahi kuwaona watu weupe (Wazungu)  watatu tu,  na alikuwa hajui thamani ya fedha ya noti ,  (kwa mujibu watovuti ya Legend)  fedha ambazo angepata katika mapato yake ya kwanza katika Filamu ya THE GODS MUST BE CRAZY alikuwa tayari kuziacha zikaenda na  upepo maana hakujua matumizi yake.

Katika filamu hiyo ya kwanza mwaka 1980 alipata kiasi cha Dola 300 za Kimarekani, muda huo alifundishwa thamani ya fedha katika Ulimwengu na hivyo Filamu zilizofuata aliweza kufanya makubaliano ya kuigiza na kupata malipo makubwa kufikia Rand za Afrika kusini R800,000. Japo hakuwa na uelewa wa matumizi ya pesa bado aliweza kujenga nyumba nzuri kwa ajili ya familia yake.

Baada ya kuachana na mikataba ya kazi yake ya filamu katika mataifa mbalimbali Duniani ikiwemo China na Marekani, alirudi Namibia, ambako alilima mahindi, maboga na maharage na kufuga ng’ombe kadhaa (lakini si zaidi ya 20 wakati huo, kwa  sababu kwa mujibu wa Tovuti ya  Independent, bila mifumo ya kisasa ya kilimo yeye alikuwa anapata shida sana katika ufugaji wa ng’ombe zaidi ya hao zaidi), ila baadae jarida la Namibia liitwalo  NEW ERA lilisema kuwa hakuwa na uwezo wa kuhesabu zaidi ya 20.

Katika hatua nyingine, mwezi Julai mwaka 2000 N! XAU Aliingia rasmi katika dini ya Kikristo, na baadae alibatizwa na kuwa Mu-Adventista Msabato.

Tarehe 5 Julai 2003, alifariki kutokana na magonjwa sugu ya kifua yaliyoambatana na kifua kikuu, wakati hou  alikuwa akijihusisha na uwindaji wa ndege aina ya Kanga. Kulingana na makadirio rasmi alikuwa na umri wa miaka kati ya 58 au 59 wakati huo, na alizikwa Julai 12 huko Tsumkwe karibu na kaburi la mke wake wa pili. Na alikuwa na watoto sita waliokuwa hai.

FILAMU ALIZOIGIZA

1.      The Gods Must Be Crazy (1980) (Actor)

2.      The Gods Must Be Crazy II (1988) (Actor)

3.      Kwacca Strikes Back (1990) (Actor)

4.      Crazy Safari (1991) (Actor)

5.      Crazy Hong Kong (1993) (Actor)

6.      The Gods Must be Funny in China (1994) (Actor)

7.      Sekai Ururun Taizaiki (1996) (Himself)
Loading...