Mradi mkubwa wa kisasa wa mazingira utakaowezesha ukuaji wa miche ya miti kufuatiliwa kwa njia ya digitali umeanzishwa katika mji wa Himo ukilenga kufikia malengo ya dunia ya mwaka 2030 ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mradi huo unatekelezwa kwa pamoja kati ya Halmashauri ya wilaya ya Moshi na Serikali katika jiji la Kiel la nchini Ujerumani utagharimu zaidi ya kiasi cha Euro 58,000 ambapo sehemu ya fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuandaa vitalu kuotesha miche ya miti.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi ,Michael Kilawila alisema mradi huo uliibuliwa mwaka 2017 wakati wa mkutano wa Global Engagement uliofanyika nchini Ujerumani baada ya kuona fursa katika uanzishwaji wa vitalu vya miti kwa ajili ya kurudisha uoto uliozolekea katika mkoa wa Kilimanjaro.
