Madereva wa Bajaji Lindi watoa ya moyoni


Madereva wa Bajaji wanaoendesha katika kituo cha soko kuu Manispaa ya Lindi, ambao wamekuwa wakichukua abiria kutoka Lindi mjini hadi Mitwelo mkoani humo, wamelalamikia hali ya ugumu wa biashara hiyo kwa kile walichokieleza abiria wengi sasa wamekuwa wakitembea kwa mguu kutokana na hali ya kiuchumi kuwa ngumu.

Madereva hao wa Bajaji wamesema awali walikuwa wakipata abiria kila baada ya dakika 5 bajaji inajaza na kuondoka lakini kwa sasa bajaji moja ambayo inabeba abiria 3 inakaa mpaka masaa mawili hadi matatu ndio ijae jambo ambalo kwa bajaji zaidi ya 31 moja zilizopo katika kituo hiko zingine hukosa zamu ya kupakia kwa siku.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items