Ibrahim Hassan (7) amefariki dunia baada ya kukanyagwa jana na mashabiki waliojitokeza kuangalia mpira uwanja wa Taifa. Mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Temeke, Dar es Salaam.
Baba mzazi wa mtoto huyo amesema anampenda sana mwanae ila hakuwa na fedha ya kumnunulia tiketi, alimruhusu kwenda kuangalia japo kwa nje sababu alimuomba sana.
Vurugu hizo zilitokea jana Uwanja wa Taifa wakati wa mchezo kati ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Uganda, The Cranes ulimalizika kwa Stars kushinda 3-0.
