Naibu Waziri Dkt Ndugulile atembelea kituo cha utafiti na Maabara ya ugonjwa wa Seli Mundu


Naibu Waziri Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile (Mb) ametembelea kituo Cha Utafiti na Maabara ya ugonjwa wa Seli Mundu kilichopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Wakati akiwa katika ziara hiyo, aliwasisitiza watalaam kuhakikisha maabara hizo zinakuwa na manufaa mapana kwa wananchi ambao mara nyingi wanachelewa kujua kama wanamatatizo ya Seli Mundu na magonjwa mengine ya kurithi.

Aidha, alieleza maabara hiyo ni miongoni mwa maabara chache sana Africa Mashariki hivyo, zitumike vyema kupata matokeo chanya pamoja na kutumika kujifunza na kufanyia tafiti mbalimbali kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili.