R Kelly akanwa mchana kweupe


Baada ya Mkongwe wa muziki R Kelly kuiomba mahakama impe ruhusa ya kusafiri kwenda kupiga Show nchini Dubai, Serikali ya nchi hiyo imekanusha kuwa Kells hana Show yoyote Dubai.

Serikali ya Dubai imesema kuwa taarifa za R kelly kwenda kufanya Show nchini humo sio za kweli na wala hakuna klabu hata moja ambayo imemtafuta kwaajili ya Show. Rkelly aliomba ruhusa ya kwenda nchini humo kutumbuiza kwa madai ya kuwa imekua ngumu kwake kupata kazi nchini Marekani hasa kwasababu ya tuhuma zinazomkabili.

Apo awali ililipotiwa kuwa mkali wa R&B, R Kelly alimuomba jaji ruhusa ya kusafiri kwenda kupiga show Dubai na kudai kuwa imekuwa ngumu kwake kupata show kwa Marekani tangu tuhuma zianze kumuandama mapema mwaka huu.

Hata hivyo waandaji wengi wamemkataa na hata show zilizokuwa tayari zimeandaliwa zilihairishwa baada ya tuhuma za vitendo vya unyanyasaji wa kingono kwa mabinti wadogo kuanza kumuandama.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items