Roma na Stamina (Rostam) kuufungua mwaka 2019


Kundi la muziki wa Hip Hop Bongo linaloundwa na Roma na Stamina (Rostam) lipo mbioni kuachia wimbo wao mpya ambao utakuwa ni wa kwanza kwa mwaka huu, 2019.

Wimbo wa mwisho kutoka kwenye kundi hilo ni ule unaokwenda kwa jina la Anaolewa. Hata hivyo kwa kipindi ambacho wamekuwa kimya, Roma ameweza kushirikishwa na wasanii kama Mwasiti na Bill Nass kwenye nyimbo zao.

Pia ni kipindi kirefu kwa wasanii wa kundi hilo kutoa wimbo kama solo artist, wimbo wa mwisho kwa Stamina kutoa unaitwa Love Me aliomshirikisha Maua Sama, huku wimbo wa mwisho kwa Roma unakwenda kwa jina la Zimbwabwe.