Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Simba SC, Mohammed Dewji amesema kuwa anaamini kuwa timu ya Taifa Stas itafanya vizuri kwenye mchezo wa leo.
Utakumbuka kuwa MO Dewji ni miongoni mwa watu walioteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuwasaidia Taifa Stars ishindi mchezo wa leo dhidi ya Uganda.
"Watanzania wote tuko nyuma yenu! Tunawaamini mtafanya vizuri na kuishonyesha dunia kwamba na sisi Tanzania tunaweza," amesema MO Dewji.
Timu ya Taifa, Taifa Stars leo Jumapili inashuka kwenye dimba la uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza dhidi ya Uganda ambapo timu hiyo inahitaji kupata pointi tatu muhimu ili kuiwezesha kufuzu fainali za mataifa huru ya Afrika (AFCON) ambazo zinatarajiwa kufanyika nchini Misri.
