Tani 8 za nyama mbovu zateketezwa na serikali


Serikali imeteketeza shehena ya nyama mbovu za ng’ombe na nguruwe zenye viambata vya sumu zisizofaa kwa matumizi ya binadamu na zilizokwisha muda wa matumizi tani 8 zilizoingizwa nchini kwa njia za panya na kuhatarisha afya za wananchi.

Akizungumza wakati akishuhudia zoezi la uteketezaji wa nyama hizo Njiro jijini Arusha juzi jioni, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina alisema kukamatwa kwa bidhaa hizo ni sehemu ya matokeo ya operesheni Nzagamba iliyowezesha kukamatwa na kuteketezwa kilo 26,295 za nyama mbovu na maziwa zilizokuwa zimeingia nchini kinyume cha Sheria.

Pia nyama hizo zimekamatwa zikiuzwa katika Super Markets mbalimbali ambapo licha ya kutofaa kwa matumizi ya binadamu pia zimeingia nchini bila vibali, bila kulipiwa ushuru wa Serikali na wala kuhakikiwa ubora wake huku nyingine zikiwa hazina nembo wala taarifa yoyote katika vifungashio jambo ambalo ni hatari kwa afya za walaji.


Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items