Baba aua mtoto kwa kumyonga akidai 'amebambikiziwa'


Polisi inamshikilia Mkazi wa mtaa wa Vitendo, Kata ya Misugusugu Wilayani Kibaha, Robison Ernest(33) kwa tuhuma za kumuua mtoto, Modesta Robison(Miezi 6) akidai si mwanae.

Inadaiwa Ernest ambaye ni fundi ujenzi alifanya kitendo hicho wakati mama wa mtoto akiwa sokoni kwa ajili ya kununua mahitaji ya nyumbani.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Wankyo Nyigesa amesema baada ya Mtuhumiwa kufanya kitendo hicho mnamo Aprili 01 mwaka huu aliuficha mwili chini ya uvungu wa kitanda.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items