RC Makonda kuja na kampeni kubwa kuwasaidia kina mama Dar


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameeleza kuwa anatarajia kukutana na Wakina mama wajane, Jijini Dar es salaam, April, 04 mwaka huu ili kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili ikiwemo suala la mirathi.

Pia pamoja na kutoa elimu kwao kuhusu Asilimia 4 zinazotengwa kwa kila manispaa kwa wanawake ili wajue kuwa fedha hizi zinawahusu.

Lakini pia amewapongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Mkuu wa Wilaya ya Temeke kwa kukamilisha zoezi la ugawaji wa Vitambulisho kwa wafangabiashara wadogowadogo kwenye maeneo yao, lakini pia amewataka Wakuu wa wilaya wa Kigamboni, Kinondoni na Ubungo kuongeza kasi ya kukamilisha zoezi hilo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items