Bodi ya matibabu yawafutia usajili madaktari 2,063



Katika zoezi hilo Madaktari wa Kinywa 212 nao wamefutiwa usajili, hatua hii imechukuliwa kwa wataalamu wa sekta ya afya wanaofanya kazi katika Hospitali za Serikali na binafsi.

Imeelezwa kuwa waliofutiwa usajili walikiuka kanuni za usajili kwa kutohuisha leseni zao baada ya muda kuisha.

Madaktari nchini Kenya wanapaswa kulipa kiasi cha shilingi za kitanzania 91,500 kila mwaka kama ada ya leseni.

Hata hivyo bodi hiyo imetoa utaratibu wa kuomba upya usajili. Watakaohitaji wametaarifiwa kuwa fomu zinapatikana kwenye tovuti ya bodi hiyo.