Bugando yapata Madaktari bingwa



Hospitali ya Rufaa ya Bugando wameungana na Taasisi ya mifupa Moi, Cuba katika kambi ya upasuaji wa ubongo ,mgongo na mishipa ya fahamu ambayo ilikuwa inafanyika Mkoani Mwanza.

zaidi ya wagonjwa 400 wamehudumiwa kati yao 17 wakifanyiwa upasuaji mkubwa na jopo la madaktari hao bingwa toka tarehe 8/04/2019 hadi 12/04/2019. 

Akihitimisha kambi hiyo Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Dkt Philisi Nyimbi amemshukuru rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuri kwakufanya maboresho makubwa hapa nchini hususani kwenye huduma za afya. 

“Kambi hii ya upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu imeweza kutokana na maboresho yaliyofanya na serikali ya awamu ya tano, kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Ndg. John Mongela tunawashukuru wakurugenzi wakuu wa MOI na Bugando pamoja na madaktari bigwa wote, kwa hili wananchi wa kanda ya ziwa wamenufaika sana”. Amesema Dkt Philisi. 

Mkurugenzi mtendaji wa MOI Dkt Respicios Boniface amesema hii ni sehemu ya mkakati wa MOI na serikali kuhakikisha huduma za kibingwa zinawafikia wananchi wote hususani wa mikoa ya pembezoni. 

“Baada ya serikali kufanya uwekezaji mkubwa MOI, rufaa za nje ya nchi zimepungua sana hivi sasa wa MOI na serikali ni kuhakikisha huduma za kibigwa zinawafikia wananchi wote”. Amesema Dkt.Boniface. 


“Kwa niaba ya bodi pamoja na menejimenti ya hospitali ya Bugando tunawashukuru wenzetu wa MOI,Cuba kwa kuja kushirikiana nasi hapa kwenye kambi yah ii, tunaamini huu ni mwanzo wa ushirikiano baina ya taasisi zetu wakazi wa kanda ya ziwa wataendelea kunufaika”. Amesema Prof. Makubi.. 

Taasisi ya MOI imekuwa ikitekeleza kwa vitendo maagizo ya serikali ya kuhakikisha inawaongezea wananchi wa mikoa ya pembezoni huduma za kibigwa ili kuwapunguzia adha ya kusafiri kuzifuata 
Mpya zaidi Nzee zaidi