Bunge lampa adhabu Halima Mdee


Bunge limeazimia kumsimamisha mikutano Mmwili ya Bunge kuanzia tarehe ya azimio Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kutokana na kukiri kuunga mkono kauli ya CAG ya kusema mbunge ni dhaifu ikiwa ni mara yake ya nne kutenda makosa hayo ya kulidharau Bunge na kupewa adhabu.

Akiwasilisha azimio hilo bungeni Mwenyekiti wa kamati ya Haki Maadili na Madaraka ya Bunge, Emanuel Mwakasaka amesema Mbunge huyo alipoitwa kwenya kamati ili kujieleza alikiri kutamka maneno hayo na kuonyesha kutojutia huku akidai kuwa ni maoni yake binafsi na anao uhuru wa kutoa maoni kama mwananchi.

Pia Kamati ya Bunge ya Kinga, Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imemtia hatiani Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikal (CAG) Profesa Mussa Asadi kwa kudharau Bunge kwa kusema Bunge ni dhaifu na hivyo hawako tayari kufanya naye kazi.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items