Kumetokea ajali ya basi dogo lililokuwa limebeba Wafanyakazi wa Kambi ya Wachina wanaofanya kazi ya ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera leo April 02/2019 majira ya asubuhi.
Taarifa zinaeleza watu watatu wanasadikiwa kufariki na majeruhi wamekimbizwa Hospitali ya Murugwanza na Nyamiaga kwa matibabu zaidi.


