Freeman Mbowe ambana Waziri Bungeni


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi amesema hali ya usalama nchini ni
salama na vurugu zilizotokea katika mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Namanga zilishughulikiwa na vyombo husika na kumalizwa.

Ameeleza hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe aliyeuliza nini chanzo cha   vurugu zilizotokea mpakani mwa Tanzania na Kenya, Namanga hivi karibuni.

"Hivi karibu katika mpaka wa Namanga, tulishuhudia kupitia vyombo vya habari vurugu kubwa zilizofanywa kupitia upande wa Kenya, unatupa tamko gani kama waziri kuhusu usalama wa nchi yetu katika mpaka ule na nini kilitokea," aliuliza Mbowe.

Mkutano wa 15 wa Bunge umeeanza leo April 02, 2019 Jijini Dodoma ambapo wastani wa maswali 515 ya kawaida yataulizwa na kujibiwa na serikali. Aidha, wastani wa maswali 88 ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa kwa siku ya alhamisi.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items