UEFA yaipiga rungu Chelsea na Malmo


UEFA leo wamefikia maamuzi magumu ya kuviadhibu vilabu vya Chelsea na Malmo kufuatia makosa ya mashabiki wake yaliooneshwa wakati wa mchezo wa 32 bora ya UEFA League Februari 14 nchini Sweden.

Mashabiki wa pande zote mbili wamesababisha timu zao zipigwe faini kutokana na kutenda makosa ambayo hayatakiwi mchezoni, Chelsea wameadhibiwa kwa kupigwa faini ya pauni 11,000 (Tsh milioni 33) kwa kosa la mashabiki wao kuvamia uwanjani.

Wakati Malmo FC wenyeji wa mchezo huo waliopoteza mbele ya Chelsea kwa mabao 2-1, wamepigwa faini ya pauni 49,000 (Tsh Milioni 147 ) kwa kosa la mashabiki wao kurusha miale ya moto (fireworks) uwanjani wakati mchezo ukiendelea.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items