Wabunge wa upinzani wasusa na kutoka nje kisa Halima Mdee


Wabunge wa upinzani wametoka nje ya bunge kupinga hatua iliyochukuliwa na Bunge ya kumsimamisha Halima Mdee mikutano miwili ya bunge kuanzia leo kutokana na kulidharau Bunge.

Leo Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge pia imemtia hatiani Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kwa kulidharau Bunge kwa kuunga mkono kauli ya CAG kuwa Bunge ni dhaifu na hivyo apewe adhabu ya kutoudhuria mikutano miwili ya Bunge.

Mkutano wa 15 wa Bunge umeeanza leo April 02, 2018 Jijini Dodoma ambapo wastani wa maswali 515 ya kawaida yataulizwa na kujibiwa na serikali. Aidha, wastani wa maswali 88 ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa kwa siku ya alhamisi.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items