Kamati ya Maadili Haki na Madaraka ya Bunge imemtia hatiani Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kwa kulidharau bunge.
Kufuatia hatua hiyo Kamati imetoa mapendekezo ya Bunge kutofanya kazi na CAG,Prof.Asaad
Kamati hiyo imesema Prof. Assad alikiri mbele ya kamati kuliita Bunge dhaifu lakini alipingana na tafsiri ya neno 'dhaifu' iliyopo kwenye Kamusi ya Kiswahili Sanifu inayosema 'goigoi, hafifu, isiyo imara' akisitiza kiuhasibu udhaifu ni 'upungufu'.
Utakumbuka CAG alipokuwa akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa na alisema,'Kama tunatoa ripoti zinaonyesha kuna ubadhirifu halafu hatua hazichukuliwi, hupo kwangu ni udhaifu wa Bunge,'.
