Serikali watofautiana juu ya fedha za mgodi(MRAHABA)


Na Timohty Itembe Mara.

Naibu Waziri Serikali za mitaa Tami semi,Mwita Waitara amesema kuwa fedha zilizokuwa zigawanywe katika halmashauri za Mkoa Mara mchakato huo umesimamishwa na kuwa fedha hizo zinatakiwa kubaki Tarime na kufanya maendeleo ya Taime na sio vinginevyo.

Waitara alisema hayo juzi alipokuwa akihutubia  wananchi wa mkutano wa hadhara uliofanyikia ndani ya  viwanja vya shule ya msingi Sabasaba iliyopo halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara.

Naibu waziri aliongeza kuwa fedha hizo zinatakiwa  kubaki na kufanya shuguli za maendeleo ya Tarime na siovinginevyo pia aliongeza kuwa badala yake Halmashauri ya Tarime Vijijini inatakiwa kutenga fedha kwaajili ya kuunga mkono upungufu wa vifaa tiba na madawa uliopo ndani ya hospitali ya wilaya inayomilikiwa na halmashauri ya Tarime Mjini.

“Nipende kusema kuwa serikali imekaa na kukubaliana kuwa fedha ya Mrahaba inayotoka Mgodi wa Nyamongo haitagawanywa kama ilivyokuwa imetangazwa hapo nyuma na mkuu wa mkoa Mara badala yake fedha hiyo itabaki kama ilivyokuwa hapo nyuma ili kufanya shuguli za maendeleo ndani ya Tarime ila halmashauri ya Tarime Vijijini inatakiwa kutenga fedha kwaajili ya kuunga mkono halmashauri ya Tarime mjini kwaajili ya kununulia madawa na vifaa tiba katika hospitali ya wilaya kwasababu watuwake wakiugua  wanakuja kutibiwa hapo”alisema Waitara.


Awali  mkuu wa mkoa Mara,Adamu Kigoma Malima alitangaza  kuwa fedha ambazo zinatolewa na Mgodi wa ACACIA kama kodi ya ushuru wa huduma ya jamii ndani ya halmashauri ya Tarime kuna haja zigawanywe katika halmashauri zote  zinazounda mkoa Mara.

Kauli hiyo ya Malima ilikuja baada ya kuituhumu halmashauri ya Tarime kuwa imepokea fedha zaidi ya Bilioni 9.5 kwa miaka mitatu na  kuwa matumizi yake hayaendani na mapokezi ya fedha hizo.

Naye mkurugenzi wa halmashauri ya Tarime vijijini,Apoll Tindwa alikiri kupokea agizo hilo na kuwa watalitekeleza kwa wakati ambapo aliongeza kuwa  tayari wametenga shilingi milioni 400 kukabidhi halmashauri ya Mji wa Tarime ili kuunga juhudi za Elimu na Afya.

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Tarime.Elias Ntiruhungwa alisema kuwa wanayo mapungufu mengi ndani ya hospitali ya wilaya inayomilikiwa na halmashauri yake ikiwemo upungufu wa madawa na vifaa tiba kutokana na wingi wa wagonjwa wanaokuja kutibiwa hapo.

Ntirugungwa alifafanua kuwa hospitali hiyo inapokea wagonjwa wengi kutoka Wilaya  za Serengeti,Rorya,Halmashauri ya Tarime mji na Tarime vijijini,huku wagonjwa   wengine wakipokelewa kutoka Nchi jirani ya Kenya  ambapo kwa hali hiyo  hospitali hiyo inalemewa na msalaba mzito wa Wagonjwa wanaokuja kutibiwa hapo.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items