Wakati Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), ikitangaza uchaguzi mdogo wa ubunge Arumeru Mashariki kufanyika Mei 19, Chama cha Demokrasia na Maendeleo, kupitia Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Vicent Mashinji amesema chama hicho hakitashiriki uchaguzi huo kwa kile alichodai ni kupoteza muda.
Uchaguzi huo utafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CHADEMA, Joshua Nassari kuvuliwa ubunge wake na Spika Job Ndugai kutokana na kutohudhuria mikutano ya bunge mitatu mfulululizo bila kutoa taarifa yeyote .
Utakumbuka Machi 14, 2019 Spika wa Bunge Job Ndugai, alitangaza kumvua Nassari ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kwa makosa ya mahudhurio hafifu bungeni ikiwemo kukosa vikao vya mikutano mitatu ya Bunge.
