Huyu ndie Nipsey Hussle, msanii aliyepigwa risasi Marekani


Ni mwanamuziki wa Rap na muandishi akitokea Los Angels, California Marekani. Majina yake kamili ni Ermias Davidson Asghedom ameishi duniani kwa kipindi hiki (August 15, 1985 – March 31, 2019) pekee.

Alichipukia kutoka kundi la West Cost HipHop tangu katikati ya miaka ya 2000, Jamaa alijulikana kwa Mixtapes zaidi na hizi ni baadhi tu ya Mixtapes alizowahi kutisha nazo Bullets Ain't Got No Name series, The Marathon, The Marathon Continues and Crenshaw.

Mwaka 2018 aliachia Album yake ambayo aliipa jina Victory Lap, hii ilikuwa mwezi Fubruari, mafanikio yalikuwa makubwa kwa Album hiyo, jamaa aliuza copies nyingi na baadae akawa blessed kuingia kwenye kipengele cha Best Rap Album kwenye tuzo za kila mwaka, ikiwa mara ya 61 kufanyika Academy Grammy mwaka2019.

Alikuwa akifanya kazi na label za muziki za All Money In, Atlantic, Cinematic pamoja na Epic.

Amefariki siku ya 31/3/2019 kwa kupigwa risasi huko Los Angels, California.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items