Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amewataka viongozi wa sekta ya afya katika halmashauri ya Iringa vijijini kuendelea kutundika bendera nyekundu kwa wananchi ambao hawana vyoo bora ili kutumisha usafi na afya kwa wananchi wote.
Akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wananchi,Viongozi, Taasisi na Jumuiya mbalimbali kwa kutekeleza vizuri kampeni ya kuwa na vyoo bora ambavyo vimeipa ushindi halmasahuri ya Iringa Vijijini kwa kupata tuzo ya usafi hapa nchini.
Kasesela alisema kuwa ofisi ya afya katika halmasahuri ya Iringa Vijijini wamekuwa wakisimamia vizuri swala la afya na kuwa na vyoo bora ambapo wanataraji kuwa halmashauri ya kwanza kwa kuwa na vyoo bora kuliko halmashuri zote za mkoa wa Iringa hadi taifa.
“Nampongeza bibi afya wa hapa amekuwa mkali kuhakikisha hakuna mtu anayeweza kukwamisha zoezi lolote la kuboresha sekta ya afya na kuhakikisha afya za wananchi wa wilaya hii wanakuwa na
afya njema” alisema Kasesela
Aidha Kasesela amepiga marufuku wa wazazi kujifungulia majumbani kwa kuwa sio sehemu salama kwa uzazi wa mtoto wakati serikali imefanikiwa kuboresha sekta ya afya ambayo ndio kipaumbele cha serikali ya awamu ya tano.
“Jukumu la kwanza kwa baba ni kuhakikisha amempeleka mama kliniki kupata huduma ili kuwa na malezi mazuri ya mtoto, hivyo tutaondoa ile njia ya akinamama kujifungulia majumbani kwa kuwa
tayari baba atakuwa anajua wajibu wake,” alisema Kasesela
Kasesela amewataka watendaji wa kata,vijiji na maafisa tarafa kuhakikisha hakuna mama anajifungulia nyumbani na nitamshughulikia mtendaji yeyeto Yule ambaye hata wachukulia hatua akibaba watakao fanikisha mama kujifungulia numbani.
Awali akitoa hutuba kwa mgeni rasmi mkurugenzi wa halmasahuri ya Iringa Vijijini Robert Masunya aliwataka watendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha wameendeleza juhudi hiyo ya kuhakikisha wananchi wote wanakuwa na vyoo bora ili kupunguza na kumaliza tatizo la milipuko ya magonjwa.
