Yanga SC kuifuata Ndanda kesho


Jumla ya wachezaji 20 wa kikosi cha Yanga SC, kesho alfajiri wataanza safari ya kueleka Mtwara tayari kwa mchezo wa ligi dhidi ya wenyeji Ndanda FC, mchezo uliopangwa kutimua vumbi, April
4 kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Afisa habari wa timu hiyo Dismas Ten amesema kuwa Nahodha Ibrahim Ajib ataendelea kukosekana  kikosini kupisha majeraha madogo aliyo nayo huku Juma abdul akirejea kikosini baada ya kupona majeraha yake.

“Ibrahim Ajib bado tutaendelea kumkosa kikosini kutokana na majeraha ya mguu,lakinijambo jema ni kwamba Juma Abdul amerejea kikosini na atakuwa sehemu ya msafara wa kikosi chetu,mchezo utakuwa mgumu lakini maandalizi tuliyoyafanya yanatosha kutupa matokeo mazuri”. alisema Dismas Ten
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items