Na. Ahmad Mmow,Lindi
Wazazi na walezi mkoani Lindi wameombwa kufuatilia maendeleo ya watoto wao kielimu, maadili na kuchangia ujenzi wa miundo mbinu ya kutolea elimu.
Wito huo umetolewa leo na mjumbe waa baraza kuu la taifa la Jumuia ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), Meta Naonyo alipokuwa anazungumza na wazazi na walezi kwenye zoezi la kujitoa katika ujenzi wa shule ya sekondari Kilangala, iliyopo katika wilaya ya Lindi.
Naonyo alisema Jumuia ya Wazazi ya CCM, pamoja na mambo mengine inashughulikia masuala ya maadili na malezi. Ambapo kila mwaka ufanya makongamano na kufanya shughuli za kijamii ikiwa ni maadhimisho ya kuanzishwa Jumuia hiyo. Ambapo mwaka huu imefikisha miaka 64 tangu kuanzishwa kwake.
Alisema wazazi wanawajibu kuchangia ujenzi wa miundo mbinu ya elimu kwa kutumia rasilimali fedha, nguvu, mali na muda ili kuharakisha na kurahisisha upatikanajii elimu bora kwa watoto. Kutokana na mazingira rafiki ya kujifunza na kufundishia
"Tumeamua kushiriki kufyatua tofali na kuchangia mifuko 20 ya saruji. Ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali za kutoa huduma kwa wananchi," alisema Naonyo.
Maadhimisho ya mwaka huu kimkoa yalifanyika katika wilaya na mji wa Nachingwea. Ambayo yaliwashirikisha viongozi wa Jumuia hiyo kutoka katika wilaya zote tano zinazounda mkoa wa Lindi.
