Kocha wa Simba SC awaweka kiporo TP Mazembe


Kocha Mkuu wa Simba SC, Patrick Aussems amesema kwasasa hafikirii mechi dhidi ya TP Mazembe kwasababu bado ana mechi moja mkononi ya Ligi Kuu Soka Tanzania (TPL) Jumatano kabla ya kuhamia kwenye majukumu ya kimataifa. .

Kikosi cha Simba SC kitashuka dimbani Jumamosi ya Aprili 6 mwaka huu kuwaalika TP Mazembe katika mechi ya mkondo wa kwanza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kuhusu mchezo wa jana dhidi ya Mbao FC, kocha huyo amesema, 'Kila mechi tunacheza kushinda, hata huu mchezo tulistahili kushinda, tulianza kushambulia tangu mwanzo hadi mwisho, mchezo ulikuwa mgumu lakini tulitengeneza nafasi'.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items