Kwa kuripoti unyanyasaji wa kingono achomwa moto hadi kufa


Nusrat Jahan Rafi alimwagiwa mafuta ya taa na kuchomwa moto Shuleni kwake katika mji wa Bangladesh, yapata wiki mbili kabla alikuwa amewasilisha malalamiko ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya mkuu wake wa Shule..

Ushupavu wake wa kuweka wazi unyanyasaji wa kingono ulisababisha kifo chake kwa kuchomwa moto na kuibua hisia tofauti miongoni mwa raia wa Bangladesh na kuonyesha namna waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono wanavyokabiliwa na hatari katika taifa hilo lenye itikadi kali lililopo kusini mwa bara la Asia.

Nusrat ambaye alikuwa na umri wa miaka 19, alikuwa anatoka katika mji mdogo wa Feni, uliopo maili 100 kutoka mji mkuu Dhaka, Alikuwa anasoma katika shule ya Kiislamu ya madrassa na Machi 7 alisema kuwa Mkuu wa shule alimuita ofisini kwake na kumtomasa. Kabla mambo hayafika mbali alikimbia nje ya ofisi.

Wasichana wengi na wanawake wenye umri mdogo nchini Bangladesh huamua kunyamaza kimya wanapofanyiwa unyanyasaji wa kingono au kubakwa kwa kuhofia kudhalilisha jamii au familia zao, Kilichofanywa tofauti na Nusrat Jahan ni kwamba hakuzungumzia suala hilo kwa sauti tu bali alikwenda pia kwa polisi kwa msaada wa familia yake katika siku ambayo unyanyasaji huo ulidaiwa kufanyika.

Katika kituo cha polisi mjini humo kilieleza kuwa Alitakiwa kupewa mazingira salama ili aweze kutathmini yaliyomtokea, Badala yake alichukuliwa video na afisa wa polisi husika kupitia simu yake huku akielezea yaliyompata.

Katika video hiyo Nusrat anaonekana wazi akiwa na mkanganyiko huku akijaribu kuficha uso wake kwa mikono, Polisi anasikika akisema malalamiko hayo "sio jambo kubwa " na kumueleza nusrat aondoe mikono usoni nz baadaye video hiyo ilivifikia vyombo vya habari nchini humo.