Mfanyabiashara atiwa mbaroni kwa uzembe barabarani na kuua


Na John Walter-Manyara

Mtoto mdogo wa miaka 5 mkazi wa Nangwa-Songambele wilaya ya Hanang mkoani Manyara amefariki dunia mara baada ya kugongwa na gari alipokuwa akijaribu kuvuka barabara.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga amemtaja marehemu kuwa ni Frank Paskali aliekuwa akitembea kwa miguu katika barabara kuu ya Katesh-Babati ndipo alipogongwa na dereva ambaye pia ni Mfanyabiashara aitwaye Erasmus Naselim Marupa mwenye umri wa miaka 30 mkazi wa Manyoni Singida aliekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T 377 DMH aina ya Toyota Kulger na kusababisha kifo cha mtoto huyo.

Kamanda ameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva huyo kutotii sheria za bara barani.

Wakati huohuo kamanda Senga amesema, Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa mara baada ya kudondokewa na viroba vya mchanga katika Mgodi wa Yuyuu Kasago wenye Pml namba 003276NZ.

Amemtaja aliefariki kuwa ni Victor Lema [22] mkazi wa Migungani Arusha na kuwajeruhi Shadrack Elitael [21] ,Ernest Athanasio [20],Damian Martin [27] na Baraka Japhet [24] wote wakazi wa Arusha na afya zao zinaendelea vizuri.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items