DC Kabeho mgeni rasmi fainali kombe la UVCCM


Na Timothy Itembe Mara

Mkuu wa wilaya Tarime mkoani Mara,Charles Kabeho anatarajiwa kuwa mgeni rasimi katika fainali ya kombe la UVCCM linalotarajiwa kufanyika Aprili 22 mwaka 2019 katika viwanja vya mpira wa miguu Chuo cha uwalimu (TTC) na kumalizika 22 Aprili,2019.

Akiongea ofisini kwake katibu wa Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi Wilayani hapa,Newton Mongi alisema kuwa Ligi hiyo itashirikisha Timu Nane kutoka kata zinazounda halmashauri ya Mji wa Tarime Mara.

Mongi alizitaja kata  hizo ambazo zinaunda halmashauri ya Mji wa Tarime kuwa ni pamoja na kata ya Bomani,Kitare,Nyamisangura,Nkende,Turwa,Kenyamanyori,Sabasaba na Nyandoto.

Kwa upande wake katibu mhamasishaji wa Umoja wa Vijana wa Chama cha mapinduzi wilaya Tarime,Remmy Mkapa alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji kwa vijana,Kupinga na kukemea madawa ya kulevya pamoja na Vijana kujifunza Uzalendo wa kuipenda Nchi yao.

Naye katibu wa Chama cha mapinuzi wilaya Tarime,Khamisi mkaruka alisema kuwa mashindano hayo yamefadhiliwa na kada wa Chama cha mapinduzi CCM,Martini Jeradi.

“Katika mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuanza  hapo Aprili 06,2019 ndani ya viwanja vya mpira wa miguu TTC ambayo yatachezwa kwanjia ya mtoano na kuwa  fainali yake inatarajiwa kufanyika Aprili 22 mwaka huu chini ya mgeni rasimi mkuu wa wilaya Tarime Charles Kabeho ambapo mshindi wa kwaza atajishindia shilingi laki tano na Kombe huku mshindi wa pili akitoka na kitita cha shilingi laki laki tatu na mpira mmoja na mshindi wa tatu atatoka na shilingi laki mbili”alisema Mkaruka.   
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items