Mtoto aliyetekwa anyongwa hadi kufa


Mtekaji alimtaka Baba wa Mtoto Junior Bakari Siame aliyekuwa Mwanafunzi wa Darasa la 3 katika Shule ya Msingi ya Hanga atume milioni 10 ili asimdhuru.

Baba wa Mtoto alijitahidi na kumtumia Mtekaji shilingi elfu 30 lakini akaambiwa hela haitoshi utume nyingine.

Mtekaji alimtaka auze nyumba, alimuuliza kati ya Mtoto na nyumba kipi muhimu? Mtekaji alimpeleka Mtoto huyo hadi Mlima Nyoka, ambako Mtoto huyo aliuawa, hata hivyo Mtekaji amekamatwa Ipogolo, Iringa.