Muimbaji Rose Muhando aruhusiwa kutoka Hospitali


Msanii wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando hatimaye ameondoka Hospitalini nchini Kenya alipokuwa akipatiwa matibabu.

Majeraha hayaonekani tena na anaonekana ni mchangamfu mno. Katika video iliyochapishwa na Solomon Mkubwa anaonekana akiimba na kumshukuru Mungu kwa kumponya.
Muhando ambaye aliibua hisia kali miongoni mwa mashabiki wake nchini Kenya na Tanzania yapata miezi 4 iliyopita alipoonekana jijini Nairobi akiwa na majeraha na akiombewa na mhubiri wa Neno Evangelism jijini Nairobi James Nganga ameonekana akiwa na waimbaji wenza wa nyimbo za dini Betty Bayo, Solomon Mkubwa miongoni mwa wengine.