Papa Francis ahimiza amani Libya na Sudan

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ametoa mwito kwa viongozi wa dunia wa kufanya bidii kwa mara nyingine ili kuleta amani nchini Libya na Syria ambako migogoro imeathiri maisha ya watu. Akihubiri kwenye ibada ya Pasaka iliyohudhuriwa na waumini wapatao 70,000 kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro, Papa Francis pia alielezea huzuni yake juu ya mauaji yaliyotokea nchini Sri Lanka kutokana na mashambulio ya mabomu yaliyofanyika kwenye makanisa na hoteli.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani amezitaka pande zote zinazohusika na mgogoro wa nchini Libya zifanye mazungumzo badala ya kuendelea kupigana. Papa Francis amesema sasa ni wakati wa kujizatiti tena ili kuleta masuluhisho kwa njia ya mazungumzo.

Juu ya Sudan Kusini Papa Francis amewataka viongozzi wa nchi hiyo wafanye mazungumzo ya kuleta maridhiano ya kitaifa.