Rais Trump aiponda ripoti ya uchunguzi wa Muller


Rais wa Marekani Donald Trump ameziita baadhi ya taarifa zilizotolewa dhidi yake katika ripoti ya uchunguzi wa mshauri maalumu Robert Muller kuwa upuuzi mtupu.

Rais Trump ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter kwamba haikuwa na umuhimu wowote kwake kuzijibu kwa kuwa zililenga kuwafanya baadhi ya watu kuonekana wema ama yeye kuonekana mbaya.

Nyaraka zilizokusanywa pamoja zimeonyesha kuwa Serikali ya Urusi iliingilia uchaguzi wa Rais wa Marekani wa mwaka 2016 kwa kiasi kikubwa na kwa mpangilio lakini pia ziliainisha mahusiano kati ya timu ya kampeni ya Trump na Urusi.

Ripoti hiyo yenye kurasa 448 ilitaja pia takriban matukio 10 yaliyoashiria uwezekano wa Trump kuzuia uchunguzi huo ikiwa ni pamoja na alipomtaka mshauri katika ikulu ya White House kumfukuza kazi Muller, Ripoti ya Muller ilitolewa kwa umma siku ya jana baada ya takriban miaka miwili ya uchunguzi.