Rais wa Israel kuanza kuzungumza na waziri mkuu wiki ijayo


Rais wa Israel amesema mazungumzo yake na vyama vya siasa yataanza wiki ijayo, katika mchakato wa kumteua kiongozi anayefikiri ana nafasi nzuri ya kuunda muungano imara wa serikali.

Reuven Rivlin ameongeza leo kwamba, kwa mara ya kwanza, mikutano yake na viongozi wa vyama itatangazwa moja kwa moja na televisheni, kwa ajili ya uwazi.

Licha ya kuwa rais ana wadhifa ambao si wa kiutendaji, anahusika na kumteua mgombea wa wadhifa wa waziri mkuu baada ya kusikia mapendekezo kutoka kwa vikundi vyote.

 Baada ya hapo atamtaka mgombea anayeongoza kuunda serikali katika muda wa masaa 42.Waziri mkuu Benjamin Netanyahu anaonekana kuwa chaguo la rais, wakati ambapo matokeo yanayokaribia kukamilika yakitoa kwa chama cha Likud na vyama vingine vya kizalendo na vya kidini wingi mkubwa bungeni.