Rapper Nipsey Hussle afariki dunia kwa kupigwa risasi


Umeshawahi kulisikia jina la Nipsey Hussle? Basi rapper (33) huyo amefariki dunia kwa kupigwa risasi Los Angeles, Marekani.

Raper huyo ambaye amewahi kuwania tuzo ya Grammy amedaiwa kupigwa risasi mbele ya duka lake la mavazi Marathon Clothing.



Kwa mujibu wa ripoti ya imesema kuwa Nipsey alishambuliwa kwa risasi kadhaa mwilini mwake na alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitalini.

Jina kamili la rapper huyo ni Ermias Davidson Asghedom na albamu yake ya mwisho ameachia mwaka jana iliyopewa jina la "Victory Lap".
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items