.

4/15/2019

RC Makonda amtaka Mkandarasi huyu kujisalimisha Polisi


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaeam, Paul Makonda emeendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo Wilaya Kinondoni ambapo amemtaka mkandarasi wa kampuni ya Ujenzi ya Scol Construction Ltd iliyotengeneza barabara ya Biafra chini ya kiwango kujisalimisha polisi kabla ya Ijumaa ya April 19.

Itakumbukwa RC Makonda aliagiza kampuni ya Scol na Delmont kurudia ujenzi wa barabara zilizojengwa chini ya kiwango kwa garama zao zao lakini kampuni ya Delmont imekubali kurudia upya Ujenzi wa barabara ya Mabatini huku kampuni ya Scol" mkandarasi wake akikaidi agizo la kurudia ujenzi wa barabara ya Biafra jambo linaloleta usumbufu kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri.

Barabara za Mabatini na Biafra zilijengwa na kampuni za Scol na Delmont chini ya kiwango na kuharibika kabla ya kukabidhiwa kwa serikali jambo lililomkwaza RC Makonda na kutaka zirudiwe upya kwa garama ya mkandarasi husika.