Serengeti boys yachapwa 3-0 na Uganda


Kikosi cha timu ya Vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys leo kimepoteza mchezo wake wa pili mbele ya Uganda kwa kuchapwa mabao 3-0 Uwanja wa Taifa.

Michuano hii ya Afcon kwa vijana inafanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania huku mwakilishi wa Tanzania, Serengeti Boys kwa mara ya kwanza alianza kwa kuchapwa mabao 5-4 na Nigeria na leo amefungwa mabao 3-0 na Uganda.

Makosa ya safu ya ulinzi pamoja na umakini dhaifu wa mlinda mlango wa Serengeti Boys umezidi kuididmiza timu ya Serengeti Boys ambayo ipo kundi A ikishikilia mkia bila kujikusanyia pointi.

Kocha wa Serengeti Boys, Oscar Mirambo amesema kuwa ni matokeo mabaya ila wanatengeneza vijana kwa ajili ya manufaa ya Taifa wakati ujao.

Sasa Serengeti Boys wamebakiwa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Angola ili kujaribu bahati yao kama itawezekana kufuzu michuano hii endapo Nigeria atamyoosha kwa mabao mengi mpinzani wake Uganda, huku naye akitakiwa kumtwanga mabao mengi Angola.