.

4/15/2019

TAKUKURU yawatahadharisha wala rushwa,yasema adhabu miaka 20 jela


Na. John Walter,Manyara

TAKUKURU Mkoani Manyara imemfungulia mashtaka wakili wa kujitegemea  Samson Rumende kwa kushiriki kughushi mikataba ya kuuza gari lililotumika kati ya JUHIBU na mmiliki wa awali kwa lengo la kukwepa kodi ya serikali.

Akitoa taarifa ya miezi mitatu ya utekelezaji wao kwa waandishi wa habari,Naibu mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Isdory Kyando amesema jumla ya wastani wa washtakiwa kutiwa hatiani ni asilimia 66.7,ambapo Emmanuel Mark Nyambo aliyekuwa afisa utumishi wilaya ya Simanjiro alitiwa hatiani kwa kosa la matumizi mabya ya madaraka baada ya kuthibitika kuwa altoa maswali ya usaili wa ajira ya watendaji wa vijiji hapo mwaka 2015 kwa mzazi wa mmoja wa watahiniwa.

Jumla ya malalamiko 89 yaliyohusu vitendo vya rushwa pamoja na ukiukaji wa sheria na kanuni yalipokelewa na yapo katika hatua mbalimbali.

Amesema kati ya hayo majalada 13  ya uchunguzi wake ulikamilika,manne yametumwa makao makuu,saba walifungua kesi mahakamani kwa kuwa hayakuhitaji kibali cha mkurugenzi wa mashtaka na majalada  mengine mawili waajiri waliandikiwa barua za kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watuhumiwa.

Amesema uendeshaji wa mashtaka umeendelea ambapo kwa kipindi hicho TAKUKURU Manyara imesimamia jumla ya kesi mpya 11 zilizofunguliwa na kati ya hizo nne zinatokana na majalada yaliyo pata kibali kwa DPP na kesi saba zilifunguliwa bila kibali.

 Dawati la Uchunguzi na mashtaka la Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Manyara imeendelea na kazi zake ambapo kwa kipindi cha miezi mitatu imepokea jumla ya taarifa 89 ambazo kati ya hizo 13 uchunguzi wake umekamilika.

Naibu mkuu ametoa tahadhari kwa wananchi kuwa wasishiriki vitendo vya rushwa kwani adhabu yake kubwa ambayo ni mpaka kifungo cha miaka 20 jela,kwani makosa hayo yamejumuishwa kwenye marebisho ya sheria ya uhujumu uchumi.

“Mambo ya faini waliyokuwa wameyazoea yamekwishakuwa ni zao la makosa waliyoyatenda”,alisisitiza Kyando.

Kwa upande mwingine TAKUKURU kwa kushirikiana na TANESCO na Halmashauri husika  mkoani hapa imebaini baadhi ya wananchi wasio waaminifu waliongeza mazao pamoja na majengo ili kuongeza thamani ya maeneo ya maendeleo tegesha,hivyo walibaini tatizo hilo na kuzuia mali zilizopatindikizwa zisiingizwe katika uthamini huo ambao ilikuwa inafikia shilingi 325,382,465.00 ambazo zilikuwa zilipwe kwa wananchi hao.

TAKUKURU inaendelea kufuatilia matumizi ya fedha za Umma katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo mkoani hapa lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa inatekelezwa kwa kiwango kinchotakiwa na thamani ya fedha inapatikana kwa kuzuia mianya ya rushwa na upotevu wa rasilimali katika utekelezaji wake.

Aidha amesema wamejipanga kuunganisha uchunguzi wowote wa mali na makosa ya utakatishaji fedha na kwamba wamegundua kuwa watu wanapata fedha kwa misingi ya rushwa na wana kwenda kuanzisha miradi mbalimbali ili kuhalalisha fedha haramu.

Ameongeza kuwa mtu akikamtwa na  makosa ya utakatishaji wa fedha hayana dhamana hivyo wanaojihusisha na tabia hizo na wasijidanganye kuwa mali haramu zitakuwa halali.