TRA wakusanya Sh. bilioni 6.6 Tarime


Na Timothy Itembe, Mara

 Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Wilaya Tarime mkoani Mara wamekusanya zaidi ya shilingi 6.6 sawa na asilimia 92 kati ya malengo waliojiwekea kukusanya shilingi Bilioni 7.1 kwa mwaka 2019.

Akizungumza na mwaandishi wa habari Ofisini kwake Afisa wa kodi TRA Wilaya Tarime mkoani Mara,Samweli Chacha alitumia nafasi hiyo kuwaasa wafanyabiashara kuendelea kutoa ushirikiana kwenye Taasisi hiyo ili kuhakikisha kuwa wanalipa kodi ya Serikali bila kusukumwa.

Chacha alifafanua kuwa makusanyo hayo ni kwa mujibu wa sheria ya mfumo wa makusanyo ya kodi kwa viwango vilivyowekwa na serikali kukusanywa kutokana na kodi inayolipwa.

“Ikiwa mauzo hayazidi shilingi 4,000,000 hakuna kodi inayolipwa badala yake serikali imekuja na mpango mkakati kwa wafanyabiashara hao ili kwenda kuchukua kitambulisho cha wajasiliamali na ikiwa mauzo yanazidi 4,000,000 lakini hayazidi shilingi 7,500,000 kwa mwaka kodi inayolipwa ni shilingi 150,000”alisema Chacha.

Pia Chacha aliongeza kuwa ikiwa mauzo yanazidi shilingi 7,500,000 lakini hayazidi shilingi 11,500,000  kodi inayolipwa ni shilingi 318,000 na ikiwa mauzo yanazidi shilingi 11,500,000 lakini hayazidi shilingi 16,000,000 kodi inayolipwa ni shilingi 546,000 huku ikiwa mauzo yanazidi shilingi 16,000,000 lakini yahazidi shilingi 20,000,000 kodi inayolipwa ni shilingi 862,500 kwa mwaka.

Kwa upande waka Meneja TRA Wilaya Tarime mkoani Mara,Frank Lwesya alisema kuwa Wafanyabiashara wanaoanda hesabu za mizani ambao mapato yao ya mwaka yanazidi shilingi 20,000,000 wanatakiwa kuandaa hesabu za ukaguzi /taarifa za fedha katika biashara zao.

Afisa huyo aliongeza kuwa wanakumbana na changamoto mbalimbali katika kukusanya mapatoi ikiwemo maeneo ya machimbo ya madini kwa wachimbaji wadogo wadogo kutokana na uwelewa mdogo pamoja na kufanya kazi huyo majira ya usiku.