Tunaweza kufuzu hatua inayofata - Kocha wa Simba SC


Kocha Mkuu wa Simba SC, Patrick Aussems amesema kuwa anaamini timu yake itaenda kufunga goli kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya TP Mazembe.

Patrick amesema bado ana kikosi kizuri ambacho kinaweza kupata ushindi mbele ya miamba hiyo ya soka kutoka DR Congo na kusonga mbele kwenye mashindano hayo.

“Kwa kuongeza umakini zaidi nina uhakika wiki ijayo tunaweza kufunga na nina uhakika tunaweza kufuzu hatua inayofata, tulikuwa na mchezo mzuri na ninataraji mchezo mzuri zaidi tukienda DR Congo”- Kocha Patrick

Kwa matokeo ya jana ya kustoshana sare ya bila kufungana dhidi ya TP Mazembe, Simba SC wanahitaji ushindi au sare yoyote ya magoli ili kutinga hatua ya nusu fainali ya klabu Bingwa Afrika.