Urusi yaazimia kuunda 'Internet' yake


Bunge la nchi hiyo limepitisha muswada ambao ukiwa sheria, Taifa hilo llinalokadiriwa kuwa na Watu zaidi ya Milioni 140 litaunda 'Internet' yake peke yake na kuacha kutumia inayotumika duniani kwa sasa.

Muswada huo uliopitishwa kwa kura nyingi za Wabunge 307 huku 68 wakiupinga, utawasilishwa katika Bunge Kuu la Urusi ili kuidhinishwa na kisha kuwasilishwa kwa Rais Vladmir Putin kuweka sahihi ili kuufanya sheria kamili.

Mmoja wa Waandishi wa muswada huo, Andrei Klishas aliliambia Shirika la Habari la Ujerumani(DW) kuwa kuna Mataifa yenye uwezo wa kiufundi wa kuizimia Urusi huduma za 'intaneti' wakati wowote wakipenda, hivyo wanajiandaa kiufundi kuhakikisha wanajilinda.