Watu Saba mbaroni kwa tuhuma za kufanya biashara haramu ya fedha

Jumla ya wahalifu saba wamekamatwa na kufikishwa Mahakamani kutokana na tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya kubadilisha fedha za kigeni kwa njia isiyo halali.

Aidha kufuatia suala hilo,Serikali imewatahadhalisha wananchi kutojihusisha na biashara hiyo kinyume na utaratibu kwani vyombo vya usalama ikiwemo Jeshi la Polisi vimeongeza nguvu katika kuhakikisha biashara hiyo haramu inatokomezwa.

Hayo yameelezwa April mosi mwaka huu Jijini Dodoma na Waziri wa fedha na Mipango Dk.Philip Mpango,wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo pia amewahakikishia watanzania kuwa Serikali ina akiba ya fedha za kigeni ya kutosha zipatazo dola za kimarekani Bilion 4.67 hadi March 30 mwaka huu zenye uwezo wa kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi kisichopungua miezi 4.8.

“Hivyo,wasiwasi kuwa serikali inachukua hatua ya kufunga baadhi ya maduka ya kubadilishia fedha za kigeni kwa sababu haina akiba ya fedha za kigeni si ya kweli hata kidogo.”Alisema.

Waziri Mpango pia amesema kuwa kwa kipindi kifupi cha utekelezaji wa zoezi la udhibiti wa biashara ya kubadilisha fedha za kigeni,thamani ya shilingi imeimarika na upatikanaji wa fedha za kigeni katika benki za biashara umekuwa mzuri.

“Kabla ya zoezi la udhibiti wa biashara ya kubadilisha fedha ya kigeni dola ya kimarekani ilikuwa inauzwa kwa wastani wa shilingi 2,450 na baada ya utekelezaji wa zoezi hilo hivi sasa dola ya Marekani inauzwa kwa wastani wa Shilingi 2,300”Waziri wa Fedha.

Aidha kutokana na Serikali kudhibidi biashara ya kubadili fedha kiholela Waziri Mpango amesema,kwa sasa imeandaa kanuni mpya kwa ajili ya biashara ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ambazo zitaelekeza jinsi ya kuomba leseni za uendeshaji wa maduka hayo kwa mtu binafsi au taasisi yeyote na masharti ya kuzingatiwa wakati wa shughuli hizo.Na Enock Magali,Dodoma

JUMLA ya wahalifu saba wamekamatwa na kufikishwa mahakamani kutokana na tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya kubadilisha fedha za kigeni kwa njia isiyo halali.

Aidha kufuatia suala hilo,Serikali imewatahadhalisha wananchi kutojihusisha na biashara hiyo kinyume na utaratibu kwani vyombo vya usalama ikiwemo Jeshi la Polisi vimeongeza nguvu katika kuhakikisha biashara hiyo haramu inatokomezwa.

Hayo yameelezwa April mosi mwaka huu Jijini Dodoma na Waziri wa fedha na Mipango Dk.Philip Mpango,wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo pia amewahakikishia watanzania kuwa Serikali ina akiba ya fedha za kigeni ya kutosha zipatazo dola za kimarekani Bilion 4.67 hadi March 30 mwaka huu zenye uwezo wa kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi kisichopungua miezi 4.8.

“Hivyo,wasiwasi kuwa serikali inachukua hatua ya kufunga baadhi ya maduka ya kubadilishia fedha za kigeni kwa sababu haina akiba ya fedha za kigeni si ya kweli hata kidogo.”Alisema.

Waziri Mpango pia amesema kuwa kwa kipindi kifupi cha utekelezaji wa zoezi la udhibiti wa biashara ya kubadilisha fedha za kigeni,thamani ya shilingi imeimarika na upatikanaji wa fedha za kigeni katika benki za biashara umekuwa mzuri.

“Kabla ya zoezi la udhibiti wa biashara ya kubadilisha fedha ya kigeni dola ya kimarekani ilikuwa inauzwa kwa wastani wa shilingi 2,450 na baada ya utekelezaji wa zoezi hilo hivi sasa dola ya Marekani inauzwa kwa wastani wa Shilingi 2,300”Waziri wa Fedha.

Aidha kutokana na Serikali kudhibidi biashara ya kubadili fedha kiholela Waziri Mpango amesema,kwa sasa imeandaa kanuni mpya kwa ajili ya biashara ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ambazo zitaelekeza jinsi ya kuomba leseni za uendeshaji wa maduka hayo kwa mtu binafsi au taasisi yeyote na masharti ya kuzingatiwa wakati wa shughuli hizo.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items