Loading...

4/23/2019

Waziri Mwakyembe awataka waliokashifiwa na Magazeti waende mahakamani


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka watu wanaokashifiwa na magazeti wakalalamike mahakamani kwa kuwa huko ndiko haki inakopatikana.

Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo bungeni leo alipokuwa akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Pia Waziri Mwakyembe amesisitiza umuhimu wa waandishi wa Habari kuzingatia maadili katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ili kulinda tunu za Taifa.

Katika hatua nyingine amesema kwamba pamoja na kwamba watu wengi wanataka kujua alipo Mwandishi Gwanda lazima waelewe kwamba eneo alilopotelea mwandishi huyo walipotea watu wengi wakiwamo viongozi wa Serikali. Kutokana na hali hiyo Waziri huyo amesema watu wasiendelee kufuatilia mahali alipo mwandishi huyo kwa kuwa hilo ni suala dhaifu.
Loading...