Loading...

5/23/2019

BREAKING: Simba SC washushiwa kichapo kizito na Sevilla FC


Timu ya Sevilla FC kutoka Hispania imeibuka na ushindi wa magoli 5-4 dhidi ya Simba SC katika mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Magoli ya Simba katika mchezo huo yamefungwa na John Bocco dk 8, Meddie Kagere dk 14,John Bocco dk 32. Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Simba SC walikuwa mbele kwa goli 3-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote mbili ambapo Sevilla FC alifanikiwa kufunga goli la pili, dk ya 61 Clatous Chota Chama (Triple C) akaifungia Simba SC goli la nne. Hadi mchezo huo unamalizika ubao wa matokeo ulisomeka Sevilla FC 5-4 Simba SC.


Loading...