Charles Hilary atamani kufanya mahojiano na Rais Magufuli, aeleza sababu


Mtangazaji wa Azam TV, Charles Hilary amesema kuwa anatamani sana kumhoji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Charlse Hilary amesema kuwa anatamani kumhoji kwasababu waandishi wengi wakimuuliza maswali anajibu mkato ila yeye atamchokoza mpaka atoe majibu ya kueleweka.

"Mimi natakamani kumhoji Rais Magufuli, kwasasababu anapenda kutoa majibu ya mkato mkato na waandishi wengi hawamuulizi sana. Mimi natamani ni mhoji ili akijibu mkato nimchokoze mpaka atatoa majibu," amesema Charles Hillary kwenye mahojiano yake na Ritha Paulsen Show.