Diwani Babati Mjini amlilia Dkt. Mengi


Na John Walter-Babati

Imekuwa ni wiki ya majonzi kwa Watanzania baada ya kupokea taarifa ya kifo cha Dkt. Reginald Mengi 2 Mei, 2019 kilichotokea Dubai katika Falme za Kiarabu.

Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka miaka 77 huku  Wengi wakimkumbuka kwa kuwa mfanyabiashara mahiri na mmiliki wa Makampuni ya IPP Limited na IPP Institute of Technology and Innovation.

Huku viongozi mbalimbali wakimiminika kwa wingi nyumbani kwa marehemu kuwafariji wafiwa. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati Mohammed Kibiki amesema pengo la Mengi ni vigumu sana kuzibika.
Mheshimiwa Kibiki ambaye pia ni diwani wa kata ya Babati Mjini, akizungumza na Munngwana Blog&Tv, amesema Mengi amekuwa akijitoa katika kusaidia wasionacho na wenye uhitaji kwenye jamii ikiwemo walemavu na kugharamia matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo nchini India.

 Amesema kuna mengi ya Kuiga na kujifunza kutoka kwa Dkt. Reginald Mengi, ikiwemo utaratibu aliokuwa amejiwekea kila mwaka mpya unapoingia kuandaa chakula cha mchana na kula na wenye ulemavu kitu ambacho hakitasahaulika miongoni mwa Watanzania.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia