Mbunge wa Mbozi (CHADEMA), Pascal Haonga ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na polisi tangu jana alipokamatwa nje ya geti la bungeni.
Kiongozi huyo alikamatwa jana na Jeshi la Polisi jijini Dodoma, wakati akitoka kuhudhuria vikao vya Bunge vinavyoendelea.
Hata hivyo Bunge limesema Spika hana mamlaka ya kuzuia mbunge kukamatwa nje ya Bunge, ni baada ya Mbunge John Mnyika kutoa hoja leo asubuhi bungeni.
Awali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto alisema Mbunge huyo anashikilia kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mitandano.
